Mishipa ya mapafu kushoto

Mishipa ya mapafu ni mishipa inayosafirisha damu yenye oksijeni nyingi kutoka mapafuni hadi atiria ya kushoto. Ipo minne kwa jumla, yaani miwili kwa kila pafu. Jozi mbili za mishipa ya mapafu, ya juu na ya chini, zipo katika kifua. Mishipa ya mapafu ya kushoto na ya kulia hutoka mtawalia katika pafu la kushoto na pafu la kulia. Kwa wastani ina urefu wa mm 15 na kipenyo cha mm 15 na haina vali.Mishipa yote minne ya mapafu ina njia ya mlalo kuelekea sehemu ya nyuma ya atiria ya kushoto. Njia hii huinama kidogo kuelekea chini kwa mishipa ya juu. Hupitia utando wa nyuzinyuzi wa moyo ambapo hufunikwa kwa kiasi na utando serosi kisha huingia kila mmoja peke yake katika atiria ya kushoto.